Viongozi Wa ODM Kisii Wabanduliwa Na Maafisa Wapya Kuchaguliwa

Wafuasi wa chama cha ODM katika kaunti ya Kisii wamewabandua viongozi wa tawi hilo la chama cha ODM na kuwachagua maafisa wapya. Wafuasi hao wamedai kuwa viongozi waliobanduliwa niA�vibaraka wa mrengo wa Jubilee. Wafuasi hao waliandaa maandamano ya amani mjini Kisii kupinga wakisuta uongozi wa tawi la kaunti hiyo la chama cha ODM. Viongozi wapya waliochaguliwa walidai kwamba hatua hiyo iliafikiwa kwenye mkutano wa faragha. Walidai kuwa maafisa waliobanduliwa mamlakani wamepuuza chama hicho walipoongoza ujumbe hadi makazi ya naibu wa rais William Ruto huko Sugoi na pia katika ikulu ya rais kwa kigezo kwamba washauriana kuhusu maendeleo ya eneo hilo. Kundi hilo limedai kwamba limechukua usukani wa tawi hilo baada ya kumbandua mwenyekiti wa tawi hilo,A� Seneta Chris Obure, katibu wake aliyepia gavana wa kaunti hiyo, James Ongwae na katibu mtendaji, aliye pia naibu gavana Joash Maangi miongoni mwa maafisa wengine. Samuel Omwando ni kaimu mwenyekiti aliwashutumu maafisa hao kwa kukiasi chama cha ODM. Kaimu katibu mtendaji Amos Andama alidai kwamba chama cha ODM kingali dhabiti na kinamuunga mkono Raila Odinga kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao