viongozi wa NASA wapeleka kampeni zao maeneo ya kajiado

Vigogo wa muungano wa upinzani NASA, kuanzia leo watapeleka kampeini zao za kutafuta kura katika maeneo ya Rift Valley, Upper Eastern na pia Kati kati mwa Kenya.A� Vigogo hao wakiongozwa na mpeperushaji bendera ya NASA, Raila Odinga, wataanza Kampeini zao kwa kukita kambi kwenye kaunti ya Kajiado, ambako watahutubia mikutano katika maeneo yaA� Namanga na Loitokitok. Hayo yanajiri muda mfupi baada ya kampeini zao za Juma lililopita katika maeneo ya PwaniA� ambapo walihutubia mikutano huko Kwale, Malindi na Mombasa. Muungano wa NASA umejigawanya katika makundi manne ya Kampeini ili kuhakikisha ujumbe wake umeenezwa katika kila pembe ya JamhuriA� mnamo siku za kwanza za msimu huu wa Kampeini hadi kufikia wakati wa uchaguzi mkuu