Viongozi wa kiislamu wakosoa amri ya kutotoka nje Tana River

Wahubiri wa Kiislamu katika kaunti ya Tana River wameitaka serikali kutangua amri ya kuto-toka nje usiku iliyotangazwa na kaimu waziri wa usalama wa kitaifa, Dr. Fred Matiangi wakisema haifai. Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la Ma-Imam na wahubiri wa Kiislamu tawi la Tana River, Tana River, wahubiri hao wamehoji ni kwa nini amri hiyo ilitangazwa katika eneo hilo ilhali hakuna visa vya ukosefu wa usalama vilivyoripotiwa.

Hata hivyo wahubiri hao wamewahimiza wakazi wa Tana River kushirikiana na serikali katika kukabiliana na tishio la ugaidi katika eneo hilo. Dr Matianga��i alitangaza amri ya kuto-toka nje usiku katika maeneo-16 ya kaunti za Lamu, Garissa na Tana River saa chache tu baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa wa waziri wa usalama wa taifa baada ya kifo cha waziri, Joseph Nkaissery. Marufuku hiyo inafuatia shambulizi la washukiwa wa kundi la wanamgambo la Al-Shabaab katika eneo la Jima, kaunti ya Lamu ambapo watu saba waliuawa na wengine kujeruhiwa.