Viongozi wa Kiambu wataka Ngilu na Waititu kushauriana kumaliza mzozo wa biashara ya makaa

Baadhi ya  viongozi katika kaunti ya  Kiambu wametoa wito kwa Magavana  Charity Ngilu wa Kitui na Ferdinard Waititu wa Kiambu kushauriana ili kutafuta suluhu kuhusu mzozo  uliofuatia mafuruku alioweka  Gavana Ngilu kuhusu   biashara ya makaa katika kaunti ya Kitui. Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya  Kiambu  Gathoni Wamushomba na mbunge wa  Ruiru Simon Kingara hata  hivyo waliwarai wakazi wa Kiambu kutochukua hatua za kulipiza kisasi baada ya lori moja lililokuwa likisafirisha makaa kuchomwa katika kaunti ya Kitui juma lililopita. Ngilu alikariri kuwa ataendelea kudumisha marufuku ya uchomaji makaa na  uzoaji mchanga ambayo iliidhinishwa na bunge la kanuti hiyo kufuatiaa malalamaishi kuhusu uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli hizo.  Wabunge wa  Kitui walipuuzilia mbali mwelekeo wa kikabila ambao marufuku hiyo imetafsriwa, wakisema kaunti ya Kitui ina watu kutoka kabila zote nchini  wanaofanya biashara halali na kuishi kwa amani.