Uchukuzi wa bidhaa Afrika mashariki Kuimarishwa zaidi

Viongozi wa mataifa ya jumuiya ya Afrika mashariki wamekubaliana kutoa kipaumbele kwa utekelezaji wa hatua zitakazo-hakikisha kwamba uchukuzi wa bidhaa baina ya mataifa hayo hautatizwi huku eneo hili likiendelea kukabiliana na chamko la Covid-19.

Kwenye mkutano kupitia video ulioandaliwa na rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya hiyo, viongozi hao waliagiza wizara zao za afya, uchukuzi na maswala ya jumuiya ya afrika mashariki kuzindua mikakati ya kuwapima madereva mipakani kwa njia ambayo haitatatiza uchukuzi wa bidhaa baina ya mataifa wanachama.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akichangia.

Viongozi hao akiwemo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, na Salva Kiir Mayardit wa Sudan, walikiri changamoto za kibiashara zilizoko hasa mipakani  katika vita dhidi ya virusi vya Covid-19, baada ya kubainika kwamba kuna uwezekano mkubwa wa virusi hivyo kusambazwa na madereva wa malori ya masafa marefu. 

Rais Kenyatta alikariri haja kwa mataifa ya jumuiya ya Afrijka mashariki kushirikiana kwenye vita dhidi ya chamko la Covid-19.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni