Baadhi Ya Wabunge Washinikiza Polisi Kuwashurutisha Viongozi Wa CORD Kuandikisha Taarifa Kuhusu Kifo Cha Jacob Juma

Baadhi ya wabunge katika Kaunti ya Kiambu wanashinikiza idara ya polisi iwashurutishe viongozi wa muungano wa CORD kuandikisha taarifa kutokana na matamshi yao kuhusu kifo cha mfanyibiashara maarufu Jacob Juma. Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, mwenzake wa Kabete, Ferdinand Waititu na Kimani Ichunga��wa wa Kikuyu wametoa wito kwa inspekta jenerali wa polisi, Joseph Boinett kuwalazimu viongozi hao wa CORD wakiongozwa na Raila Odinga kuandikisha taarifa kuhusiana na matamshi yao. Walisema wameghadhabishwa na matamshi ya viongozi hao wa CORD hasa ya kumhusisha naibu wa rais William Ruto na mauaji ya mfanyibiashara huyo aliyezikwa mwishoni mwa wiki katika eneo la Bumula, kaunti ya Bungoma. Ichunga��wa alitoa wito wa kuharakisha uchunguzi kuhusu kifo cha Juma ili waliohusika wachukuliwe hatua. Wakati uo huo, wabunge hao wamesema tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC itavunjwa endapo muungano wa CORD utazingatia utaratibu unaofaa. A�