Viongozi kutoka Elgeyo Marakwet wakubaliana kushirikiana katika kuwafurusha wezi wa mifugo

Viongozi kutoka Kaunti  za  Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi wamekubaliana kuendesha shughuli za pamoja za amani  na kuwaondoa wezi wa mifugo katika eneo hilo kufuatia  msururu wa visa vya ukosefu wa usalama kwenye sehemu hiyo.    Wajumbe kwenye mkutano wa amani uliofanyika eneo la mpakani  la  Kokwo Kalya ambapo jamii zote ziliwakilishwa  waliazimia kuunga mkono  doria za polisi wa kitaifa wa ziada ambazo zinalenga kukabiliana na ukosefu wa usalama katika sehemu hiyo. Viiongozi hao waliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi kwa amani  na kushirikiana na maafisa wa polisi waliopelekwa katika sehemu hiyo ili kumaliza ukosefu wa usalama.  Mashambulizi ya majambazi yamekuwa yakiongezeka katika sehemu hiyo  na kusababisha maelfu ya  watu kuhama makwao baada ya nyumba zao kuteketezwa majuma mawili yaliopita  kwenye mpaka wa kaunti za Pokot-Magharibi  na  Elgeyo Marakwet. Serikali imeimarisha usalama katika eneo hilo ili kurejesha hali ya kawaida