Vinara wa NASA wakubaliana kudumisha uongozi wa kamati za bunge

Vinara wa mrengo wa The National Super Alliance-NASA jana walikutana na kukubaliana kudumisha uongozi wa kamati mbalimbali za bunge kama ulivyo kwa sasa. Baada ya mkutano uliodumu kwa takriban saa tano, kiongozi wa chama cha ODM Raila OdingaA� National Super Alliance, wenzake Kalonzo Musyoka wa chama cha wiper, Musalia Mudavadi wa chama cha ANC na A�Moses Wetang’ula A�wa chama cha Ford Kenya pia walikubaliana kuendeleza mipango ya kumuapisha Raila tarehe 31 mwezi huu. A�Duru zaarifu kuwa viongozi hao wanne pia walikubaliana kuhusu haja ya kufanya mazungumzo na chama cha Jubilee kuhusu maswala ya marekebisho ya sheria za uchaguzi na kupanua serikali baada ya kurekebisha A�katiba. A�Awali chama cha Jubilee kilikuwa kimesisitiza kuwa hakitafanya mazungumzo yoyote kuhusu kugawana mamlaka isipokuwa yale yanayohusu maswala ya maendeleo. Serikali ya Marekani imeashiria kuwa tayari kufanikisha mazungumzo baina ya pande hizo mbili