Uturiki Yaahidi Kuwachukulia Hatua Washambulizi

Nci ya Uturuki imeapa kulipiza kisasi dhidi ya washambuliaji wa mlipuko mkubwa wa bomu katika mji mkuu wa Ankara,ulioacha watu 28 maiti na wengine na majeruhi 61.Rais Recep Tayyip Erdogan alisema Uturuki itafanya juhudi zote kuhakikisha usalama wake.Maafisa wamesema kuwa gari lililojaa vilipuzi lililipuliwa A�mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita siku ya jana. Hakuna kundi lolote kufikia sasa lililodai kutekeleza shambulio hilo. Marekani ilishtumu kitendo hicho na kuahidi kusimama na Uturuki.Mlipuko huo ulitokea katika eneo la karibu na bunge na makao makuu ya jeshi.