Utawala Wa Trump Umeapa Kuizuia China Kunyakua Visiwa Vinavyozozaniwa

Utawala wa rais mpya wa Marekani Donald Trump uliapa siku ya jumatatu kwamba utaizuia  China kunyakua visiwa vinavyozozaniwa kwenye bahari ya South China,huku vyombo vya habari vya China vikionya kuwa jambo hilo huenda vikazua vita.Matamshi hayo yalitolewa na hatibu wa ikulu ya Marekani ,, na yaliashiria msimamo mgumu ambao Marekani itazingatia mnamo siku zijazo,kinyume na ilivyokuiwa zamani.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani  Rex Tillerson alisema siku ya Ijumaa kuwa China haitaruhusiwa kuvinyakua visiwa hivyo vinavyogombaniwa.Matamshi ya Tillerson yalionesha kuwa huenda Marekani ikazuia  jambo hilo kupitia nguvu za kijeshi na kusababishas hofu ya kuzuka kwa mzozo na taifa la China lenye nguvu za kinyuklia.Bunge la seneti la Marekani llimemwidhinisha  Tillerson kuwa waziri wa mashauri ya kigeni,licha ya uhusiano wake wa kibiashara na Russia.