Utawala Wa Donald Trump Wakashifu Vyombo Vya Habari

Watu mashuhuri katika utawala wa rais Donald Trump wamegubikwa kwenye A�malumbano mapya na vyombo vya habari. Siku ya jumamosi rais Trump alishutumu vyombo vya habari kwa kuripoti idadi ndogo ya watu waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.Mkuu wa ikulu ya White House Reince Priebus alisema kuna watu wamepania kuharamisha uongozi wa Trump A�na kuwa hataruhusu kamwe njama hiyo kuendelea.Hata hivyo kwa mujibu wa picha za maktaba sherehe ya kuapishwa kwa aliyekuwa rais Barack Obama mnamo mwaka 2009 ilikuwa kubwa kuliko ile ya walioudhuria uapisho wa Trump.Trump alidai kuwa zaidi ya watu milioni moja na nusu walihudhuria sherehe hiyo ,lakini hakutoa uthibitisho wowote.Alipotembelea makao makuu ya A�idara ya ujasusi-CIA ,Trump aliwaelezea wanahabari kuwa watu wasioaminika.Wakati huo huo A�wataalamu wa maswala ya A�maadili na mtandao wa Wikileaks walisema jana kwamba watamshitaki rais Trump kwa ukiukaji wa maadili,hasa kuhusiana na kushindwa kuwasilisha rekodi A�za utozwaji ushuru.Tayari kampeini hiyo imeidhinishwa kwa saini 100,000.Rufaa hiyo ilianza kutayarishwa siku ya ijumaa muda mfupi baada ya kuapishwa kwa Trump kuwa rais.