Utawala nchini Malawi watoa kibali cha kukamatwa kwa aliyekua rais wa taifa hilo Joyce Banda

Utawala nchini Malawi umetoa kibali cha kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo A�Joyce Banda kuhusiana na madai ya kutumia vibaya mamlaka na makosa mengine ya ulanguzi wa pesa katika kipindi cha miaka miwili ambapo alikuwa mamlakani. Madai hayo yamekanushwa na hatibu wa Banda. Kwa mujibu wa A�msemaji wa kikosi cha taifa cha polisi James Kadadzera, makosa anayodaiwa kutekeleza Banda ni sehemu ya sakata pana ya ufisadi iliyofichuliwa mwaka wa A�2013 ambapo maafisa wakuu wa serikali wanadaiwa kuiba mamilioni ya pesa kutoka kwa serikali. Katika taarifa, hatibu huyo wa polisi alisema kuwa uchunguzi umepata ushahidi muhimu dhidi ya A�Banda. Banda ambaye aliongoza Malawi kwa miaka miwili kutoka mwaka wa A�2012, aliondoka nchini humo baada ya kupoteza uchaguzi kwa rais wa sasa A�Peter Mutharika mwaka wa 2014. Haijulikani aliko kwa sasa.