Raila Atoa Wito Kwa Waliotimu Umri Wa Miaka 18 Kuhakikisha Wanapiga Kura

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amekamilisha ziara yake katika kaunti ya Kakamega huku akitoa wito kwa maeneo bunge ambayo hayakumpigia kura katika uchaguzi mkuu uliopita yafikirie tena msimamo wao. Raila alitoa wito kwa wakazi kujiandikisha kuwa wapigakura na kuhakikisha watashiriki katika uchaguzi mkuu ujao. Alisema ,marekebisho ya hivi majuzi katika utaratibu wa uchaguzi yatahakikisha kuwa wakenya wote waliotimu umri wa kupiga kura wanaweza kufanya hivyo bila kuchelewa kama ilivyokuwa wakati uliopita katika kupata stakabadhi hiyo.

Raila pia aliulaumu utawala wa jubilee kwa kile alichokitaja kuwa ufisadi uliokithiri katika serikali. Alisema maoni yake kuwaA´┐Ż nchi hii huenda ikapoteza mabilioni ya pesa zilizopatikana kupitia mpango wa hati za dhamana za Yuro yamethibitishwa na taarifa ya Mkaguzi mkuu wamahesabu iliyowasilishwa bungeni inayoonyesha kwamba huenda shilingi bilioni 200 zilipotea.

Kiongozi huyo wa ODM sasa anaelekea huko Pwani kuungana na vinara wengine katika sherehe za kuadhimisha miaka kumi tangu kubuniwa kwa chama cha chungwa. Raila anatarajiwa kurejea katika kaunti ya Kakamega katika muda wa wiki mbili zijazo kukamilisha ziara yake katika maeneo bunge ya Lugarina Likuyani.