Utalii kuimarishwa ili kufungua biashara na awekezaji jijini Mombasa

Wadau wa sekta ya utalii mjiniA� Mombasa wametoa wito wa kukamilishwa haraka kwa miradi mikuu ya maendeleo ili kufungua maeneo ya mashambani kwa biashasra na uwekezaji. Wadau hao wamesema upanuzi wa barabara ya Airport-Port Reitz, ujenzi wa barabara kuuA� ya safu mbili ya Mombasa-Mariakani, barabara ya mkato ya Dongo-Kundu na ile ya mkato ya kaskazini mwaA� Mombasa utaimarisha ustawi wa kijamii na kiuchumi katika kaunti ya Mombasa na kurahisisha usafiri wa watalii na pia kupunguza visa vya kuchelewa kwa safari za ndege. Katika siku za hivi majuzi wauzaji wa vyakula na matunda wanaotumia barabara ya Mombasa-Nairobi wamekumbwa na hali ya kuchelewa ambayo mara nyingine iliwasababishia hasara. Watalii pia hawajasazwa huku wengi wao aghalabu wakikosa kusafiri. Barabara kuu ya mkato ya Dongo Kundu ya umbaliA� wa kilomita 18 itaunganisha eneo laA� Mombasa Mainland West na Mombasa mainland South na ni sehemu ya mpango wa awamu tatu ya kupunguza mrundiko katika mji wa Mombasa kufikia mwaka 2018.