Mahakama imedumisha ushindi wa rais Kenyatta

Mahakama ya juu imedumisha kwa kauli moja matokeo ya marudio ya uchaguzi wa urais ya tarehe 26 Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi na kwamba alichaguliwa kwa njia halali. Katika uamuzi uliochukua muda mfupi A�na kusomwa na jaji mkuu David Maraga, mahakama ilitupilia mbali rufaa za aliyekuwa mbunge wa Kilome John Harun Mwau na pia wa wanaharakati A�Njonjo Mue na Halef Khalifa kama zisizo na uzito wowote.

Hata hivyo Justice Maraga alisema kwa kuzingatia muda mfupi uliokuwepo, haingewezakana kuandika uamuzi kamili, lakini akaahidi kuwasilisha uamuzi huo katika muda wa siku 21. Pande zote za rufaa hizo zitalipia gharama zao.

Aliyekuwa mbunge wa Kilome John Harun Mwau, na pia wanaharakati Njonjo Mue na Halef Khalifa walikuwa wamewasilisha rufaa tofauti kwenye mahakama ya A�juu, kutaka kufutilia mbali uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta, kwa misingi kwamba uchaguzi huo ulighubikwa na kasoro nyingi na kamwe haukuzingatia sheria.