Usalama waimarishwa eneo la Baragoi

Usalama umeimarishwa katika eneo la Baragoi, kaunti ndogo ya Samburu Kaskazini baada ya jaribio la wizi wa mifugo liliosababisha mauaji ya mtu mmoja huku mwingine akijeruhiwa. Kulingana afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya Samburu Alfred Ageng’o, washambuliaji hao walivamia manyatta moja ya mtu wa jamii ya Samburu.A� Mwendazake anayeaminika kutoka katika jamii ya waturkana alishambuliwa na wakazi wakati wa shambulizi hilo la saa nane usiku katika kijiji cha Bendera . Washambuliaji hao wawili waliokuwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK 47 walikabiliwa na wakazi walipojaribu kuiba mifugo usiku. Ageng’o, ametoa wito wa utulivu miongoni mwa wakazi akisema usalama umeimarishwa katika eneo hilo ili kuepusha mashambulizi zaidi.