Usalama umeimarishwa Kasarani kabla ya kumuapishwa kwa Rais Uhuru

Usalama umeimarishwa katika Uwanja wa Michezo wa A�Kimataifa wa Moi A�Kasarani kabla ya shughuli ya kumuapisha Rais A�Uhuru Kenyatta na naibu wake A�William Ruto A�kwa muhula wa pili A�hapo kesho.A� A�Maafisa wa A�Usalama ambao wamejihami A�wamekuwa wakikagua kila kona ya uwanja huo hivi leo A�kuhakikisha maandalizi bora kwa shughuli hiyo A�ya kesho. A�Maafisa wa kijeshi walikuwa leo asubuhi wakikamilisha A�mazoezi ya shughuliA�A� A�ya kumuapisha Rais A�itakayohusisha A�gwaride la A�heshima. Mkuu wa wafanyakazi wa umma Joseph Kinyua, amekariri kwamba A�hatua kabambe za usalama A�zimewekwa A�kuwahakikishia Wakenya na wageni usalama A�watakapohudhuria sherehe hiyo. A�Zaidi A�ya Marais 20 na wageni wengine wa mashuhuri wa kimataifa A�wamethibitisha kuhudhuria sherehe hiyo. A�Rais Kenyatta anatarajiwa kula kiapo cha A�Urais kati ya A�saa nne asubuhi na saa nane alasiri A�kwa mujibu wa katiba. A�Sherehe hiyo haitahusisha A�kumpokeza vifaa vya kuashiria A�uongozi kwani ni rais anayehudumu.