Usalama umeimarishwa katika mahakama ya juu

Usalama uliimarishwa nje ya mahakama ya juu huku raia na waendeshaji magari wakielekezwa kutumia barabara zingine. Maafisa wa usalama waliweka vizuizi kwenye barabara ya Wabera na City Hall Way huku wakitumia vifaa vya kisasa kuchunguza hali ya usalama. Polisi walitumia kamera za CCTV kuchunguza hali ilivyo. Magari ya maafisa wa kutuliza ghasia pia yalishika doria kwenye barabara karibu na mahakama ya juu. Walioruhusiwa kuingia katika mahakama hiyo walikaguliwa kabla ya kuruhusiwa kuingia. Awali maafisa wa muungano wa NASA walibishana na afisa mmoja mkuu wa polisi alipowazuia kuingia katika mahakama ya juu lakini baadaye wakakubaliwa kuingia.