Usalama waimarishwa kwenye mpaka wa Meru na Isiolo

Hali ya utulivu inaendelea kurejea kwenye mpaka wa kaunti za Meru na Isiolo baada ya mapigano ambapo watu 10 waliuwawaA� na wengine zaidi ya elfu-tatu kulazimika kuhama makazi yao. A�Akiongea na wakazi, kamishna waA� kaunti ya Meru Wilfred Nyagwanga amewahakikishia usalama wakazi, akisema serikali imewapeleka maafisa zaidi wa usalama katika eneo hilo kudumisha amani katika eneo la mpaka kati ya kaunti za Meru na Isiolo. Kadhalika alisema wataandaa mikutano ya amani katika eneo hilo,akiongeza kuwa wamemwalika mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano kitaifa a��NCIC Francis Ole Kaparo kusaidia kupatanisha eneo hilo .Waliohama makazi yao sasa wamepiga kambi katika shule ya St. Dominica��s. Wamesema hawatarudi nyumbani hadi usalama utakapoimarishwa. Wakati huo huo wahisani, wanasiasa na shirika la msalaba mwekundu wametoa msaada wa blanketi, magodoro na chakula kwa familia zilizoathirika.