Usajili wa makurutu wa jeshi la ulinzi wa taifa waanza leo

Shughuli ya usajili wa makurutu  wa jeshi la ulinzi wa taifa  itaanza leo kote nchini na inataraajiwa kutamatishwa  tarehe 13 mwezi Machi.Naibu wa mkuu wa jeshi la ulinzi Jenerali Joseph Kasaon anatarajiwa kuzindua shughui hiyo kwenye makao makuu ya jeshi la ulinzi la taifa katika mtaa wa Hurlingham hapa Nairobi.Wale ambao wangependa kushiriki katika zoezi hilo wameonywa kuwa watatiwa nguvuni na kushtakiwa ikiwa watajaribu kutoa hongo au kufanya vitendo vyovyote  vya ufisadi wakati huo.Mtu yeyote atakayepatikana akitumia vyeti,vitambulisho vya taifa au vyeti vya masomo  ghushi, atatiwa nguvuni na kushitakuwa,kwa mujibu wa ilani ilio kwenye tangazo kuhusu shughuili hiyo.