Urusi yaonya Marekani kulenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria

Urusi imeonya Marekani kuwa itawalenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria iwapo vikosi vya kijeshi vya Urusi vitashambuliwa tena huku Marekani ikifichua kuhusu mkutano wa ana kwa ana kati ya majenarali wa Marekani na Urusi unaonuia kuepushaA� makabiliano kama hayo.A� Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema kuwa wanamgambo wa vikosi vya kidemokrasia vya Syria wanaoungwa mkono na Marekani, wamejikita katika maeneo ya Mashariki ya Syria pamoja na vikosi maalumu vya Marekani na kushambulia mara mbili vikosi vya kijeshi vya serikali ya Syria vinavyoshirikiana na vikosi maalumu vya Syria . Onyo la Urusi lilipuuza taharuki inayozidi kutanda nchini Syria kati ya Marekani na Urusi .