Urusi Yakashifiwa Kwa Mauaji Syria

Zaidi ya watu 50 wameuawa kwenye shambulizi la makombora dhidi ya shule na hospitali kaskazini mwa Syria,kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.Miongoni mwa maeneo yaliolengwa ni hospitali ya shirika la madaktari wasio na mipaka-MSF,ambako imearifiwa watu saba waliuliwa. Ufaransa imesema kuwa mashambulizi hayo A�ni uhalifu wa kivita.Wanaharakati wameishutumu RussiaA� kwa kutekeleza mashambulizi hayo,japo jambo hilo halijathibitishwa.Russia imekuwa ikiunga mkono serikali ya Syria katika vita vyake dhidi ya waasi nchini humo,huku ikidai kuwa inalenga kile ilichodai kuwa ngome za magaidi.