Urusi kuchuana na Ureno katika mechi ya kombe la mashirikisho

Wenyeji wa mashindano ya kuwania kombe la mashirikisho la soka duniani Urusi watachuana na Ureno katika mechi yao ya pili kundini kesho.Urusi iliilaza New Zealand mabao mawili kwa bila katika mechi yao ya ufunguzi kundini ambapoA� Michael Boxall na Fyodor Smolov walifunga bao moja moja. Ureno kwa upande mwingine ilipigiwa upato kuipiku Meksiko laikini ikatoka sare mabao mawili kwa mawili katika mechi ya ufunguzi. Mara ya mwisho timu hizi kuchuana ilikuwa mwaka 2015 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki ambapo Urusi iliibuka mshindi bao moja kwa sifuri dhidi ya Ureno mfungaji akiwa Roman Shirokov. Ureno itamtegemea mshambulizi wake Christiano Ronaldo ambaye alifunga bao na kuchangia ufungaji wa bao jingine timu hiyo ilipotoka sare na Meksiko mabao mawili kwa mawili. Mashindano hayo yanajumwisha timu nane zilizogawanywaA� katika makundi mawili. Meksiko iko kundini a�?Aa�� pamoja na Ureno, New Zealand na wenyeji Urusi. Kundi a�?Ba�� lina Chile, Kameruni, Ujerumani na Australia.