Upungufu wa Uwindaji Haramu Nchini

Wadau katika sekta ya mazingira wamesifia kupungua kwa visa vya uwindaji haramu hapa nchini. Kulingana na shirika la uhifadhi wanyama pori-KWS, visa vya uwindaji haramu katika mbuga za Tsavo Mashariki na Tsavo Magharibi vimepungua kwa asilimia-98 baada ya ndovu-100 kuuawa hapa nchini mwaka uliopita. Naibu mkurugenzi wa shirika la KWS Kapteni Robert Oa��brien alisema visa vya uwindaji haramu kwa kutumia bunduki vimepungua kwa asilimia-100 huku uwindajji wa kutumia mishale na nyuta ukipungua kwa asilimia-98. Mnamo mwaka 2014, Kenya ilipoteza ndovu wapatao elf-1 kutokana na uwindaji haramu akiwemo mojawapo wa ndovu wakubwa zaidi barani Afrika aliyejulikana kutokana na pembe zake kubwa na ambaye alikuwa na umri wa miaka 45. Mwenyekiti wa shirika hilo Richard Leakey alisema hali hiyo imesababishwa na kubuniwa kwa adhabu kali kwa wawindaji haramu.

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta itazindua shughuli ya kuwahesabu ndovu katika kaunti hiyo baadaye mwaka huu huku shirika la KWS likitoa wito wa kuimarishwa kwa sekta ya utalii ili kuiwezesha kaunti hiyo kujiongezea mapato.