Upinzani Waweka Masharti Ya Kuondoa Kesi Mahakamani

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amekariri kwamba upinzani uko tayari kuondoa kesi uliowasilisha mahakamani kupinga ukaguzi wa sajili ya wapiga kura mradi tu tume huru ya uchaguzi na mipaka ikutane na wadau wengine ili kujadilia malalamishi yao.Akiongea katika eneo la eastland jijini Nairobi A�wakati wa ibada ya jumapili,Kalonzo alisema ipo haja ya kulainisha sajili hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.Kalonzo amesema hayo huku eneo la kati kati mwa mkoa wa mashariki likiripoti idadi ndogo ya usajili wa wapiga kura.