UNICEF yasema watoto elfu 26 waliovuka Mediterranean walinajisiwa na walanguzi

Shirika la UNICEF linasema takriban watoto elfu-26 waliovuka bahari ya Mediterranean bila kuandamana na wazazi wao walinajisiwa au kudhulumiwa na walanguzi. Umoja wa mataifa unatahadharisha kuwa idadi kubwa ya watoto wanahatarisha maisha yao wanaposafiri kutoka nchini Libya kuelekea Italy. Hali hii ni sawa na ile inayowakumba wahamiaji kutoka barani Afrika kuelekea bara Uropa. Mwaka 2016, zaidi ya wahamiaji elfu-180 wengi wao wakiwa watoto walisafiri kwa mashua kutoka nchini Libya kuelekea Italia kupeuka ghasia zinazoshuhudiwa nchini humo. Ili kuepuka dhuluma dhidi ya watoto, Umoja wa Mataifa umehimiza Libya na mataifa jirani kubuni mashirika ya kutoa ulinzi kwa watoto.