Umoja wa mataifa umezindua mikakati ya kukabiliana na dhulma za kimapenzi

Umoja wa mataifa umezindua mikakati mipya inayolenga kukabiliana na dhulma za kimapenzi zinazotekelezwa na maafisa wa vikosi vyake vya kudumisha amani. Mikakati hiyo inajumuisha kukosa kuwalipa mishahara wanajeshi wanaochunguzwa kwa kuhusika na uhalifu huo. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema katika ripoti ya kila mwaka kuwa kuna jumla ya visa 145 vya dhulma za kimapenzi zinazohusisha wanajeshi na raia katika jumbe zote za kudumisha amani za umoja wa mataifa mwaka wa A�2016 kutoka visa A�99 mwaka wa 2015.A�

A�