Umati wakusanyika Barcelona kwa kesi ya Catalonia Artur Mas

Maelfu ya watu walikusanyika nje ya mahakama katika mji wa Barcelona nchini Uhispania wakati wa kuanza kwa kesi dhidi ya kiongozi wa zamani wa eneo la Catalonia Artur Mas. Mas anakabiliwa na shtaka la kuvuruga amani wakati wa kura ya maamuzi ambayo haikuidhinishwa ya kujiondoa kwa eneo la Catalonia kutoka utawala wa Uhispania mwezi Novemba mwaka 2014. Viongozi wa mashtaka wanataka Mas azuiwe kushikilia wadhifa wowote wa uongozi kwa miaka kumi. A�Mas, naibu wake Joana Ortega na aliyekuwa waziri wa elimu wa jimbo hilo Irene Rigau wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kuvuruga amani na kufuja pesa za umma. Wakereketwa wametumia fursa hiyo kuendeleza kampeni za kujiondoa kwa jimbo hilo huku serikali ya Uhispania ikitarajiwa kuandaa kura ya maamuzi kuhusiana na suala hilo mwezi Septemba mwaka huu.