Ulimwengu Waadhmisha Siku Ya Kifua Kikuu

Ulimwengu leo umedhimisha siku ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ulimwenguni . Shirika la afya duniani WHO limetoa witoA� kwa serikali na washikadau kuungana ili kuuangamiza ugonjwa huu unaosababisha vifo vya takriban watu milioni 1.7 kila mwaka. Kulingana na uchunguzi uliofanywa na shirika hilo mwaka waA� 2014, India ina idadi kubwa ya wagonjwa wa Kifua Kikuu ulimwenguni ikiwa na jumla ya wagonjwa milioni 2.2. Nigeria inaongoza barani Afrika ikiwa na wagonjwa 570,000. Kulingana na mkuu wa idara ya Kifua KikuuA� Daktari Enos Masini ,karibu watu 100,000 huambukizwa ugonjwa huu kila mwaka humu nchini. Enos aliongeza kuwa ugonjwa huu umeshikilia nambari nne kwa magonjwa yanayosababisha maafa nchini. Hata hivyo, idadi hii imeendelea kupungua kutokana na juhudi za serikali ya Kenya na washikadau. Kenya Imeorodheshwa kama mojawapo ya nchi ishirini zilizo na visa vingi zaidi vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ulimwenguni. Serikali ya Kenya imeanzisha utafiti kubaini takwimu kamili za visa vya ugonjwa huu humu nchini.