Ukur Yattani anawashtumu wahadhiri wanaogoma kwa kuweka vikwazo

Waziri wa lebaA� Ukur Yattani anawashtumu wahadhiri wanaogoma kwa kuweka vikwazo katika mazungumzo ambayo yangesitisha mgomo huo. Yattani alisema kuwa wahadhiri hao wamechukuwa msimamo mgumu na wanaweka matakwa yasiyowezekana. Waziri hata hivyo amesema kuwa serikali imejitolea kusitisha mgomo huo ambao umekatiza masomo katika vyuo vikuu sita vya umma kwa majuma sita. Wahadhiri kwa upande mwingine wanaishtumu wizara hiyo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.A� Waziri alisema kuwa amekuwa akifanya mikutano ya kila juma na mwenzake wa elimu A�Amina Mohammed na maafisa wa chama hicho kutoka sekta mbalimbali katika juhudi za kutafuta suluhu ya muda mrefu.