Ukavu Waendelea Kuzidi Maeneo Mbalimbali Nchini Kenya

Hali ya ukavu inatarajiwa katika maeneo mbalimbali nchini. Eneo la Nairobi na viunga vyake linatarajiwa kushuhudia vipindi vya jua kwa siku nzima huku viwango vya jua vikitarajiwa kuwa kati ya nyuzi 11 na 26. Huko A�Kisumu na viunga vyake vipindi vya jua vinatarajiwa kwa siku nzima huku viwango vya joto vikitarajiwa kuwa kati ya nyuzi 18 na 32. Hali sawa hiyo inatarajiwa katika eneo la pwani huku viwango joto huko Mombasa vikitarajiwa kuwa kati ya nyuzi 33 na 22.