Ukame wazidi Turkana Mashariki huku juhudi za kunusuru mifugo zikiendelea

Wachungaji katika kaunti ndogo ya Turkana Mashariki wananga��anga��ania malisho ya mifugo huku halmashauri ya kitaifa ya kukabilianaA�A�na ukame ikiimarisha mpango wa kunusuru mifugo kutokana na ukame. Halmashauri hiyo inalenga kunusuru kondoo na mbuzi elf-7 huku ukame unaokithiri katika kaunti ukiripotiwa kusababisha vifo vya zaidi ya mifugo laki moja. Katika kijiji chaA�Lopii ambacho kimeathirika zaidi, naibu chifu wa kata yaA�Lopii John Ebenyo alishangazwa na mamia yaA�A�wachungaji wanaotafuta malisho. Ebenyo alisema wana orodha ya wale walionufaika na mpango huo lakini orodha hiyo haikutumiwa kwa sababu wachungaji wote wamekisikitika kwa kupoteza mifugo wao kutokana na ukosefu wa malisho. Mshirikishi wa halmashauri hiyo katika kaunti hiyo Abdikadir Jillo alisema mbali ya kutoa malisho ya mifugo wameanzisha mpango wa kununmua mifugo kutoka kwa wafugaji na mpango wa kufadhili makundi yasiyojiweza . Jillo ameongeza kuwa hadi sasa asilimia 30 ya mifugo katika kaunti hiyo wamekufa huku takriban watu laki tano wakikabiliwa na njaa na kwa sasa wamesajiliwa katika mpango wa utoaji chakula cha msaada. Ukame unaokithiri katika kaunti yaA�A�Turkana umesababisha zaidi ya wachungajiA�A�40,000 kuingiaA�A�nchiniA�A�Uganda kutafuta maji , chakula na malisho ya mifugo.