Ujerumani na denmark watoka sare ya bao moja kwa moja katika mechi ya kirafiki

Mabingwa wa soka duniani Ujerumani, walitoka sare na wenyeji Denmark bao moja kwa moja katika mchuano wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa uwanjaniA� Brondby nchini Denmark, jana usiku.Denmark ilianza kufunga bao katika dakika ya 18 kupitia kwa kiungo wa timu ya Tottenham,Christian Eriksen. Ujerumani ilisawazisha zikiwa zimesalia dakika mbili mechi hiyo ikamilike kupitia kwa mlinzi wa timu ya Bayern Munich, Joshua Kimmich. Mchuano huo uliandaliwa kuadhimisha miaka 25 tangu DenMark ilipotwaa ubingwa wa kombe la Bara Ulaya mwaka 1992. Katika matokeo ya mechi nyingine za kirafiki, Ukraine ililazwa na Malta bao moja kwa nunge nayo Israel ikatoka sare na Moldova bao moja kwa moja.