Uingereza imesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Zambia

Uingereza imesitisha ufadhili wake kwa Zambia baada ya serikali ya taifa hilo kukiri kuwa Uro milioni 3.3 zilizonuiwa kusaidia familia maskini zilipotea. Haya yanafuatia madai ya ufisadi yaliyoripotiwa kuizonga serikali ya rais Edgar Lungu.

Idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza imesema kuwa taifa hilo haliwezi kuvumilia visa vya ufujaji wa pesa na ufisadi.  Mataifa ya Ireland, Finland na Sweden pia yamesitisha ufadhili wake kwa taifa hilo.

Zaidi ya asilimia hamsini ya raia wa Zambia wapatao milioni  17 wanaishi katika hali ya umaskini kwa mujibu wa benki ya dunia.