Wabunge waunga kuchaguliwa kwa jubilee ili kuendeleza miradi

Wabunge 12 wa Jubilee wameelezea hofu kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ya Jubilee huenda ikasitishwa iwapo muungano wa NASA utachukua mamlaka ya uongozi.Chini ya vugu vugu la Uhuruto Express,wabunge hao walitaja miradi ambayo huenda ikaathirika kama ile ya kupanua reli ya kisasa ya SGR hadi Naivasha. Wabunge hao kutoka sehemu mbali mbali nchini walitoa wito kwa wakenya kijitokeza kwa wingi kuipigia kura serikali ya Jubilee.Hayo yaliibuka baada ya wabunge hao kuzuru vituo kadha vya kibiasharaA� huko NaivashaA� na Gilgil katika kumpigia debe rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.Wakati wa ziara hiyo,wabunge hao walikashifu ghasia zinazoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo nchini wakiongeza kuwa kila mwanasiasa ana haki ya kufanya kampeini zake kokote nchini.Mbunge wa Naivasha kaskazini John Kihagi alitaja upanuzi wa reli hiyo ya kisasa kuwa muhimu kwa uchumi wa taifa hili.Mbunge wa Gilgil Mathenge Nderitu alitoa wito kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC kuhaikisha kuwa uchaguzi mkuu ujao unafanyika kama ilivyo pangwa.