Uhuru na Raila washinikizwa kuzungumza

Shinikizo la kutaka mazungumzo yafanywe kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga linazidi kushika kasi huku balozi wa marekani humu nchiniA�Robert Godec akiwa wa hivi punde kupaza sauti yake. Godec amesema wawili hao wanapaswa kuzungumza ili kuunganisha taifa hili ambalo linajaribu kujikwamua kutokana na joto jingi la kisiasa ambalo lilisababisha wakenya kugawanyika katika misingi ya kikabila.

Kulingana na Godec ni kupitia kwa mazungumzo ambapo maswala kuhusu uchaguzi yanaweza kushughulikiwa kikamilifu. Godec alikuwa akiongea alipokutana na Spika wa Bunge la Seneti Kenneth Lusaka ambaye alisisitiza kwamba majadiliano yanayopendekezwa yanafaa kufanyika kuambatana na katiba.