Uhuru na Naibu wake watarajiwa kukutana na viongozi wa bunge

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanatarajiwa kukutana na viongozi wa bunge hii leo ili kujadili ajenda za bunge huku wabunge wakitarajiwa kwenda likizo. Rais anatarajiwa kuwapa wabunge idhini ya A�kamati ya uteuzi ambayo itawasaili mawaziri mwaka ujao. Kamati hiyo itaongozwa na A�spika wa bunge la taifa Justin Muturi. Bunge hilo la kitaifa pia linatarajiwa kuandaa masharti na muelekeo ambao utatumiwa na kamati hiyo katika uteuzi. Kamati ya uteuzi huwachagua wabunge katika kamati mbali mbali za bunge ,ambazo idadi ya wanachama wake itaongezwa kutoka 17 hadi 19. Hakuna mbunge anayestahili kuwa mwanachama wa A�zaidi ya kamati 2. Rais Kenyatta anatarajiwa kuteua baraza la mawaziri litakaloendeleza malengo ya chama cha jubilee kwa kuimarisha utendakazi wake na maendeleo kwa jumla.