Rais Kenyatta kuzuru kaunti za Kiambu na Narok

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru kaunti ya Kiambu inayokisiwa kuwa ngome yake kwa mikutano ya kampeni huku kampeni za uchaguzi zikifikia tamati kesho. Viongozi wa chama cha Jubilee wanatarajiwa kuwarai wapiga kura wapatao milioni 1.2 wa kaunti hiyo kuwaunga mkono. Kabla ya kuzuru kaunti hiyo, mashirika mbalimbali yakiongozwa na baraza la kitaifa la makanisa na mashirika ya kijamii yalifanya maandamano mjini Kiambu kuwahimiza wakazi kudumisha amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu. Kutoka Kiambu rais anatarajiwa kuzuru kaunti ya Narok baadaye leo.