Uhuru kuongoza taifa kuadhimisha mwaka wa 39 tangu kufariki kwa Mzee Jomo Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta leo asubuhi ataliongoza taifa kuadhimisha mwaka wa 39 tangu kufariki kwa mwanzilishi wa taifa hili Mzee Jomo Kenyatta. Kwenye taarifa hatibu wa Ikulu Manoah Esipisu alisema rais anatarajiwa kuweka shada la maua katika kaburi la hayati Mzee Jomo Kenyatta katika eneo la majengo ya bunge kama ilivyo desturi. Hii itafuatiwa na ibada ya ukumbusho katika kanisa la St. Stephana��s kwenye barabara ya Jogoo saa tatu asubuhi. A�Rais wa kwanza wa jamhuri hii, marehemu Mzee Jomo Kenyatta alifariki tarehe 22 Agosti mwaka wa 1978 huko Mombasa.