Uhuru Kenyatta na Raila Odinga wakutana

Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi waA� NASA Raila Odinga wamekutana na kushauriana katika jumba la Harambee jijini Nairobi kabla ya waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson kuwasili hapa nchini .Wakiongea na waandishi wa habari baada ya mkutano huo wa faragha,viongozi hao wawili walitoa wito wa kudumishwa amani na kuahidi kushirikiana katika kushughulikia matatizo yanayoikumba nchi hii . Raila alisema mkutano huo unaashiria mwanzo mpya kwa nchi hii,matamshi yalioungwa mkono na rais Kenyatta aliyesema kuanzia jumamosi ijayo yeye pamoja na kiongozi huyo wa upinzaniA� wataanzisha harakati za kuwapatanisha Wakenya.