Uhuru kenyatta asisitiza makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza haja iliyopo kwa kundi la mataifa ya Africa, Carrebea na Pacific-ACP kupewa nafasi zaidi katika soko la muungano wa ulaya. Rais alisema mipango kama ile ya makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi yapasa kutambua kiwango cha maendeleo cha kila nchi ili kusiwe na nchi inayohisi kubaguliwa. Rais Kenyatta alisema kwamba mataifa ya Africa , Carribea na Pacific yamo katika viwango tofauti vya maendeleo na yanaweza tu kufaidika kikamilifu na mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi ikiwa viwango vyao vya maendeleo vitatiliwa maanani. Rais alisema haya leo katikaA�A�Ikulu ya Nairobi alipokutana na ujumbe wa mataifa ya Africa, Carribea na Pacific na muungano wa Ulaya ulioongozwa na Joseph Owona Kono, rais wa bunge la pamoja la mataifa ya Africa, Carribea na Pacific na muungano wa ulaya na Michele Rivasi ambaye ni rais mwenza wa bunge hilo.A�A�Rais alisema nchi hii inashinikiza hatua ya utangamano zaidi ambao utalipa bara hili usemi zaidi kwenye mashauriano yake na mashirika kama vile muungano wa ulaya huku ikitambua kiwango cha maendeleo ya kiuchumi chaA�A�kila taifa.