Uhuru Kenyatta apongeza juhudi za vikosi vya jeshi kwa kupambana na magaidi

Rais Uhuru Kenyatta amepongeza juhudi za vikosi vya jeshi la Kenya KDF kwa kupambana na magaidi nchini Somalia, na hapa nchini. Rais alilipongeza jeshi kwa jukumu wanalotekeleza katika msitu wa Boni, kaunti ya Lamu kama sehemu ya kikosi cha mataifa mbali mbali kukabiliana na magaidi na wahalifu wengineo katika kanda hii. Alisema maandalizi yao yamedidimiza uwezo wa kundi la Al Shabaab. Akiongea jana wakati wa gwaride ya kufuzu ya makurutu katika shule yao ya mafunzo huko Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu Rais Kenyatta, ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Kenya alisema moja ya kazi yake muhimu kama amiri jeshi mkuu ni kuwalinda wakenya na kulinda umoja wan chi hii kuambatana na katiba.

Hivyo basi Rais Kenyatta aliwahimiza Wakenya wote kuiga mfano wa vikosi vya nchi hii vinavyoihudumia nchi kwa kujitolea na bila kuhoka.