Uhuru azindua manifesto ya Jubilee

Rais A�Uhuru Kenyatta jana jioni alizindua manifesto ya chama cha Jubilee ambapo alifafanua mafanikio yaliyoafikiwa na serikali yake katika ajenda yake ya mageuzi na A�yale inayonuia kutimiza A�katika muda wa miaka mitano ijayo ili kuhakikisha Kenya inafikia kiwango cha taifa la mapato ya kadri .Chama hicho kilizindua mpango wa malengo A�kumi ya kuimarisha ajenda ya mageuzi yaliyokitwa kwenye msingi wa nguzo tatu. Manifesto hiyo inajumuisha kubuniwa kwa nafasi milioni A�1.3 za ajira kila mwaka na kushirikiana na serikali za kaunti kujenga angalau kiwanda kimoja katika kila kaunti, kuanzisha mpango utakaofadhiliwa na serikali wa utoaji mafunzo kwa wanafunzi wote watakaohitimu kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kiufundi kwa hadi miezi 12 ,A� kuongeza mara dufu idadi ya wakenya wasiojiweza wanaonufaika kupitia mpango wa kufadhili makundi yasiyojiweza wa Inua Jamii kutoka laki saba hadi milioni 1.4. A�Makundi haya yatajumuisha wakenya wote waliotimizaA� umri wa miaka sabini . Vile vile wakenya wote waliotimiza A�umri wa miaka sabini watanufaika naA� bima ya kitaifa ya matibabu . Aidha chama cha jubilee kimeahidi kupanua mpango wa utoaji elimu ya shule ya msingi bila malipo ili kujumuisha utoaji elimu ya shule za kutwa za umma bila malipo hapa nchini. Kadhalika chama cha Jubilee kimeahidi kupanua utoaji huduma za kina mama kujifungua bila malipo ili kujumuisha bima ya kitaifa ya matibabu inayofadhiliwa na serikali kwa kila mama mja mzito kwa muda wa mwaka mmoja. Chama cha A�Jubilee kitahakikisha kila mkenya anaunganishiwa umeme kwa bei nafuu kufikia mwaka 2020 miongoni mwa maswala mengine. A�Rais amesema chama cha Jubilee kimejitolea kutatua matatizo ya wakenya tofauti na upinzani ambao unaeneza lawama na propaganda tupu. Kwa upande wake naibu rais A�William Ruto alisema manifesto ya chama cha Jubilee ni manifesto bora zaidi ambayo wakenya wanaweza kupata kutoka kwa chama chochote cha kisiasa na inaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika muda wa miaka minne unusu A�iliyopita.