Uhuru Azindua Magari Mapya Ya Polisi

Rais Uhuru Kenyatta leo alizindua magari mapya ya polisi na vifaa vilivyonunuliwa na serikali ya kitaifa kupitia mpango wa uboreshaji vitengo vya polisi. Rais alizindua magari-525 yakiwemo-25 yasioweza kulipuliwa na mabomu ya kutegwa ardhini katika bustani ya Uhuru Park jijini Nairobi. Baadhi ya magari hayo yalinunuliwa kutoka kampuni ya General Motors East Africa ambayo itarekebisha na kudumisa magairi hayo. Magari hayo yatatumiwa katika shughuli za kila siku za udumishaji usalama katika kaunti kadhaa, kaunti ndogo na miji. Magari-2,220 yalizinduliwa katika awamu ya kwanza na pili ya mpango huo.