Uhuru awashukuru maafisa wa usalama na familia zao

Rais Uhuru Kenyatta ameahakikishia maafisa wa usalama nchini serikali itaendelea kuwaunga mkono ili kuwawezesha kuwahudumia wakenya ipasavyo. Akiongea wakati wa maombi na ibada ya pamoja ya kutoa shukrani ya maafisa wa usalama na familia zao iliyoandaliwa katika kanisa la Holy Family Basilica, Nairobi, Rais alisema ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha vikosi vyote vya usalama vimepewa vifaa vya kisasa na mafunzo ya hali ya juu na ushughulikia maslahi yao kikamilifu.Aliwashukuru maafisa hao kwa kujitolea mhanga kuihudumia nchi hii akisema Kenya ni salama na thabiti kwasababu yao huku akiwapongeza wale walipoteza maisha yao wakitekeleza majukumu yao ya kuilinda nchi hii. Ibada hiyo iliongozwa na right Reverend Salesius Mugambi,askofu wa Meru ambaye pia ni askofu wa maafisa wa uslama.Ibada hiyo ya kila mwaka ilihudhuriwa na maafisa wa polisi wa kawaida, wa Utawala, maafisa wa C.I.D, askari wa magereza, kwas shirika la ulinzi wa misitu na wa NYS.