Uhuru atembea kutoka afisi yake hadi jengo la wizara ya Afya

Rais Uhuru Kenyatta jana alizua msisimuko katika barabara ya Harambee Avenue alipotembea kutoka ofisi yake katika jumba la Harambee hadi jengo la wizara ya fedha. Wakenya waliokuwa na msisimuko walinga��anga��ana kumsalimia rais huku wachache wakiweza kumsalimia kiongozi wa nchi. Katika jengo la wizara ya fedha, rais alifanya mkutano na kundi lake la wataalam wa masuala ya kiuchumi kama sehemu ya mashauriano yake kabla ya kuratibu mpango wake wa kuendeleza ustawi wa kiuchumi wa taifa hili. Rais anatarajiwa kuratibu mpango wake wa marekebisho ya kiuchumi atakapolihutubia taifa siku ya Jumanne wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake. Mkutano huo wa jana ulikuwa wa tatu kwa rais kukutana na kundi hilo la wataalam wa masuala ya kiuchumi katika muda wa wiki tatu zilizopita. Mikutano hiyo ilianza baada ya rais kuchaguliwa tena kwenye marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 26 mwezi Oktoba kama ilivyoagiza mahakama ya juu. Kundi hilo la wataalam wa masuala ya kiuchumi tayari limemuarifu rais kuhusu sekta za maji na kawi kwenye mikutano ya awali.