Uhuru Ataka Mataifa Yazingatie Mkataba Wa Mabadiliko Tabia Nchi

 

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambao unatoa matumaini makubwa kwa mataifa yalioathiriwa na mabadiliko hayo. Rais alisema baraza lake la mawaziri tayari limeidhinisha uratibishaji wa mkataba wa Paris na sasa linasubiri idhini ya bunge. Rais Kenyatta alisema hayo mjini Marrakech, Morocco alipowahutubia wajumbe kwenye kongamano la kwanza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa baadaA�ya kongamano la kihistoria lililondaliwa mjini Paris mwaka jana. Rais alipongeza utekelezaji wa mkataba huo wa Paris akisema utashugulikia pakubwa tatizo hilo la athari za mabadiliko ya hali ya hewa. Kiongozi wa taifa alisema utekelezaji wa makubaliano hayo utasaidia kutumiza malengo ya maendeleo yakiwemo kuangamizwa kwa umaskini, utendaji haki na kusaidia kukabiliana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa na athari zake. Rais alisema ipo haja ya kuwianisha utaratibu wa utekelezaji wa mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na malengo ya maendeleo. Aliongeza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huathiri sekta za kiuchumi na kijamii hapa nchini, Rais Kenyatta alisema Kenya imetoa mchango wake katika kukabiliana na changamoto za kimazingira kupitia sheria ya mabadiliko ya hali ya hewa kuambatana na mkataba wa Paris. Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe kutoka mataifa-190 wakiwemo viongozi wa nchi na serikali mia moja.