Uhuru Apendekeza Jopo La Uteuzi Wa Makamishna Wa IEBC

Rais Uhuru Kenyatta amependekeza majina ya watu saba kwa jopo la uteuzi la tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini (IEBC), ambalo litasimamia uteuzi wa makamishna wapya wa tume ya IEBC. Hayo yanajiri siku chache baada ya makamishna wa sasa kuwasilisha barua zao za kujiuzulu; hivyo kuashiria mwanzo wa utaratibu mwingine wa uteuzi wa makamishna wapya wa tume hiyo, ambao watasimamia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Wale waliopendekezwa kwa jopo hilo la uteuzi ni:- Evans Monari, Mary Karen Kigen a��Sorobit; Jaji mstaafu Tom Mbaluto; Ogla Chepkemoi Karani; Bernadette W. Musundi; Reverend Canon Peter Karanja Mwangi; Professor Abdulghafur El-Busaidy; Askofu A�David Oginde; na Rajesh Rawal. Rais Kenyatta hata hivyo alihimiza umma kushiriki katika zoezi hilo muhimu la uteuzi wa makamishna wapya, kwa kutoa maoni yao kuhusu wale watakao-orodheshwa na jopo la uteuzi la tume ya IEBC.