Uhuru amtaka Wambugu kutupilia mbali rufaa dhidi ya Maraga

Rais Uhuru Kenyatta leo amemtaka mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri Wambugu kuondolea mbali rufaa dhidi ya jaji mkuu David Maraga,akisema kwamba kampeini za marudio ya uchaguzi wa urais ya tarehe 17 mwezi ujao ndio inayopaswa kutiliwa umuhimu. Wakati wa kongamano la viongozi wa eneo la mlima Kenya hii leo,rais alisema anaelewa machungu ya mbunge huyo kutokana na uamuzi wa mahakama kuu wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 8 mwezi jana,lakini kwa sasa juhudi zote zinapaswa kuangazia uchaguzi huo wa marudio mwezi ujao.Jana mbunge huyo wa Nyeri mjini aliwasilisha rufaa kwa tume ya huduma ya idara ya mahakama akitaka kutimuliwa kwa jaji mkuu.