Uhuru ahimiza vyuo vikuu kuhimiza ajenda ya maendeleo katika hatamu yake

Rais Uhuru Kenyatta amevihimiza vyuo vikuu hapa nchini kutekeleza jukumu muhimu kwenye ajenda ya maendeleo katika hatamu yake ya pili ya uongozi, kwa kuhakikisha kuwepo kwa chakula cha kutosha , nyumba za gharama nafuu na huduma bora ya afya .Akiongea alipoongoza sherehe ya mahafali ya chuo kikuu cha Kibabii katika kaunti ya Bungoma ambako mbunge wa Bumula Bifwoli Wakoli alihitimu shahada ya uzamili ya Elimu, rais Kenyatta alivirai vyuo vikuu kuendeleza ujuzi unaohitajika miongoni mwa wanafunzi na vile vile kuhusu ujasiriamali, akisema utasaidia kubuni nafasi za ajira. Kiongozi wa taifa alivipongeza vyuo vikuu kwa jukumu lao katika kuimarisha maendeleo humu nchini. Rais Kenyatta aliahidi kuwa utawala wake utaendelea kuviunga mkono vvyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu kwa kutoa rasilmali muhimu na vifaa ili kutoa rasilmali watu wanaohitajika humu nchini. Kwa upande wake waziri wa Elimu Fred Matianga��i alihakikisha kwamba wizara yake itaendelea kutekeleza marekebisho katika sekta ya elimu ili kuwa na ubora nay a kuaminika.